Video 1 kati ya 8
KARIBU KIJANI ASILI AFFILIATE
ANZA SAFARI YAKO YA KIJANI ASILI AFFILIATE
KIJANI ASILI AFFILIATE Kijani Asili Affiliate ni mfumo wa kidijitali unaowawezesha watu kujenga biashara na kipato kwa kuunganisha wateja na bidhaa na huduma za Kijani Asili. Lengo letu ni kujenga mtandao mkubwa wa wajasiriamali wenye maarifa, wanaotumia teknolojia, mahusiano na fursa zilizopo ndani ya Kijani Asili kufanya mauzo, kupata kamisheni na kukuza biashara endelevu.
ANZA HAPA
MAFUNZO A KIJANI ASILI AFFILIATE
Tazama kila video kwa mapngilio kuanzia ya kwanza. Kila somo limeandaliwa kukusaidia kuelewa mfumo na hatua unazopaswa kuchukua kama Affiliate wa Kijani Asili.
Explore the platform
A quick visual guide
See the important parts of the platform and read what each one helps you do.

1
KIJANI ASILI AFFILIATE NI NINI?
KIJANI ASILI AFFILIATE NI NINI? Kijani Asili Affiliate ni mfumo wa kidijitali wa biashara na ujasiriamali unaokuwezesha kujenga kipato kwa kuunganisha watu na huduma mbalimbali za Kijani Asili, ikiwemo bidhaa, ushauri wa afya, vipimo vya maabara, mipango ya lishe, mazoezi maalum na programu za afya. Kila affiliate anapata Dashboard, link na QR Code binafsi, Marketing Library pamoja na Affiliate Wallet kwa ajili ya kusimamia shughuli zake, kutangaza huduma, kufuatilia mauzo, kupata kamisheni na kutoa mapato yake. Mfumo pia unajumuisha Affiliate Challenges, zawadi, mafunzo na fursa ya kujenga timu na mtandao wa biashara. Kwa kifupi, Kijani Asili Affiliate ni mfumo unaokupa zana, huduma na fursa ya kuanza, kujenga na kukuza biashara yako kupitia Kijani Asili.

2
JINSI MFUMO WA KIJANI ASILI AFFILIATE UNAVYOFANYA KAZI
SOMO LA 2: JINSI MFUMO WA KIJANI ASILI AFFILIATE UNAVYOFANYA KAZI Mfumo wa Kijani Asili Affiliate umeundwa kukuwezesha kuunganisha wateja na bidhaa pamoja na huduma mbalimbali za Kijani Asili na kupata kamisheni kutokana na mauzo yanayostahili. Kila affiliate anakuwa na account yake binafsi, Dashboard, referral link na QR Code ambazo mfumo hutumia kutambua shughuli na mauzo yake. Mfumo unafanya kazi kwa hatua rahisi: 1. Tafuta mteja — Tumia mitandao ya kijamii, WhatsApp, marafiki, familia, sehemu za kazi, seminars au mazingira yanayokuzunguka kupata watu wanaohitaji bidhaa au huduma za Kijani Asili. 2. Tambua anachohitaji — Zungumza na mteja, msikilize na muelekeze kwenye bidhaa au huduma inayofaa mahitaji yake bila kutoa ahadi zisizo sahihi. 3. Muunganishe na Kijani Asili — Tumia link au QR Code yako binafsi kumleta mteja kwenye mfumo ili shughuli yake iweze kutambulika chini ya account yako. 4. Mteja anapata huduma au bidhaa — Anaweza kupata bidhaa, consultation, vipimo vya maabara, mpango wa lishe, mazoezi maalum au huduma nyingine zinazopatikana ndani ya mfumo. 5. Unapata kamisheni — Mauzo yanayostahili kamisheni yanapokamilika na kuthibitishwa, kamisheni yako huingizwa kwenye Kijani Asili Affiliate Wallet, ambapo unaweza kuifuatilia na kufanya withdrawal kwa mujibu wa taratibu za mfumo. Kadri unavyotafuta wateja, kufanya follow-up, kutumia Marketing Library na kujenga mtandao wako, ndivyo unavyoongeza nafasi ya kukuza mauzo na kipato chako. MFUMO NI RAHISI: Tafuta Mteja → Tambua Hitaji → Tumia Link/QR Code → Mauzo Yakamilike → Pata Kamisheni → Jenga Mtandao → Kukuza Biashara.

3
BIDHAA NA HUDUMA ZA KIJANI ASILI AFFILIATE.
SOMO LA 3: BIDHAA NA HUDUMA ZA KIJANI ASILI AFFILIATE Kama Kijani Asili Affiliate, kazi yako si kutangaza bidhaa pekee. Mfumo wa Kijani Asili una huduma mbalimbali ambazo unaweza kuunganisha na wateja kulingana na mahitaji yao. Huduma kuu zinazopatikana ni pamoja na: • Bidhaa za afya – Kutangaza na kuunganisha wateja na bidhaa mbalimbali zinazopatikana Kijani Asili Shop. • Consultation – Kuunganisha watu wanaohitaji kupata ushauri wa kitaalamu kulingana na huduma zinazopatikana kwenye mfumo. • Vipimo vya Maabara – Kuunganisha wateja wanaohitaji huduma mbalimbali za vipimo vya maabara. • Dietary Plans – Mipango maalum ya lishe kulingana na mahitaji na malengo ya mteja. • Specific Workout Routines – Programu maalum za mazoezi zinazochaguliwa kulingana na mahitaji ya mtu. • Therapeutic Routines – Ratiba na programu maalum zinazolenga kusaidia ustawi wa mteja kulingana na mahitaji yake. • Huduma nyingine za Kijani Asili – Kadri huduma mpya zinavyoongezwa kwenye mfumo, affiliate anapata fursa zaidi za kuwaunganisha wateja na huduma hizo. Kazi yako kama affiliate ni kujifunza huduma zilizopo, kutambua hitaji la mteja na kumuunganisha na huduma sahihi kupitia mfumo wako. Kadri unavyoelewa bidhaa na huduma za Kijani Asili, ndivyo inavyokuwa rahisi kutafuta wateja, kuwasaidia kufanya maamuzi na kuongeza nafasi zako za kupata kamisheni. KUMBUKA: Affiliate si daktari wala mtoa huduma isipokuwa ana sifa husika. Jukumu lako kuu ni kutangaza, kuunganisha mteja na mfumo, na kuhakikisha anafika kwenye huduma sahihi.

4
DASHBOARD,LINK NA QR CODE YAKO
SOMO LA 4: DASHBOARD, LINK NA QR CODE YAKO Kila Kijani Asili Affiliate anakuwa na Dashboard yake binafsi ambayo ndiyo kituo kikuu cha kusimamia shughuli zake ndani ya mfumo. Kupitia Dashboard unaweza kuona taarifa muhimu za account yako, kufuatilia shughuli zako, kupata Affiliate Link na QR Code yako binafsi**, pamoja na kutumia vipengele mbalimbali vilivyopo kwenye mfumo. Affiliate Link ni kiungo chako binafsi unachoweza kutuma kupitia WhatsApp, Instagram, Facebook au njia nyingine. Mteja anapotumia link yako kufanya shughuli inayostahili kamisheni, mfumo unaweza kuitambua chini ya account yako. QR Code inarahisisha zaidi kuwafikia wateja. Unaweza kumtumia mteja QR Code yako au akaiscan moja kwa moja kupitia simu yake ili kufungua huduma au bidhaa inayohusika. Unaweza kutumia Link na QR Code kwenye mitandao ya kijamii, seminars, posters, business cards, WhatsApp Status au unapozungumza moja kwa moja na potential customers. KUMBUKA: Hakikisha unatumia Link au QR Code yako binafsi unapomuunganisha mteja na mfumo ili mauzo yanayostahili yaweze kutambulika kwa usahihi. Dashboard → Chagua Huduma/Bidhaa → Share Link/QR Code → Mteja Anakamilisha Ununuzi → Mauzo Yanatambulika → Unapata Kamisheni.

5
PRODUCT SECTION NA MARKETING LIBRARY
SOMO LA 5: PRODUCT SECTION NA MARKETING LIBRARY Product Section na Marketing Library ni sehemu muhimu zinazokusaidia kufanya biashara yako ya Kijani Asili Affiliate kwa urahisi zaidi. Kupitia Product Section, unaweza kuona bidhaa na huduma mbalimbali zinazopatikana Kijani Asili, kupata taarifa zake na kutumia mfumo kumuunganisha mteja na bidhaa au huduma anayohitaji. Marketing Library ni sehemu yenye nyenzo mbalimbali za kukusaidia kutangaza. Hapa unaweza kupata picha, video na maudhui ya matangazo yaliyotayarishwa tayari kwa ajili ya kushare kupitia WhatsApp, Instagram, Facebook na majukwaa mengine. Badala ya kuanza kutengeneza matangazo yako kutoka mwanzo kila siku, tumia Marketing Library kupata content, ichague kulingana na aina ya wateja unaotaka kuwafikia, kisha share kwa consistency. Lengo ni kukusaidia kufanya kazi kwa mfumo rahisi: Chagua Bidhaa/Huduma → Pata Content → Tangaza → Pata Leads → Fanya Follow-up → Unganisha Mteja → Pata Kamisheni. KUMBUKA: Marketing Library ni chombo chako cha kutafuta wateja. Usikusanye content kwenye simu pekee — itumie kila siku kutengeneza mauzo.

6
JINSI YA KUPATA LEADS NA KUWABADILISHA KUWA WATEJA
SOMO LA 6: JINSI YA KUPATA LEADS NA KUWABADILISHA KUWA CUSTOMERS Lead ni mtu ambaye ameonesha interest kwenye bidhaa au huduma za Kijani Asili lakini bado hajafanya manunuzi. Kazi yako kama affiliate ni kumpata, kuelewa anachohitaji na kumsaidia kufikia hatua ya kufanya uamuzi. Unaweza kupata leads kupitia WhatsApp Status, Instagram, Facebook, TikTok, referrals, QR Code, seminars, marafiki, familia, sehemu za kazi na mawasiliano ya ana kwa ana. Usianze mazungumzo kwa kulazimisha mauzo. Anza kwa kusikiliza na kuuliza maswali: Ana changamoto gani? Anahitaji msaada gani? Amejaribu nini? Majibu yake yatakusaidia kujua namna sahihi ya kumuunganisha na Kijani Asili. Baada ya kuelewa hitaji lake, muelekeze kwenye bidhaa au huduma inayofaa, mtumie link au QR Code yako na msaidie kuelewa hatua inayofuata. Kama hajafanya manunuzi siku hiyo, usiache lead yako. Fanya follow-up kwa heshima. Wateja wengi huhitaji muda, taarifa zaidi au kukumbushwa kabla ya kufanya uamuzi. MFUMO WA MAUZO: Tafuta Leads → Anzisha Mazungumzo → Sikiliza → Tambua Hitaji → Toa Suluhisho → Follow-up → Funga Mauzo → Jenga Mahusiano. KUMBUKA: Affiliate mzuri halazimishi watu kununua — anaelewa mahitaji yao, anajenga uaminifu na anawasaidia kufanya uamuzi sahihi.

7
KAMISHENI,POINTS NA AFFILIATE WALLET
SOMO LA 7: KAMISHENI, POINTS NA AFFILIATE WALLET Katika Kijani Asili Affiliate, shughuli zako zinaweza kukuwezesha kupata **kamisheni, points na zawadi kulingana na taratibu za mfumo. Kamisheni ni malipo unayopata pale mteja aliyemuunganisha kupitia mfumo wako anapokamilisha ununuzi wa bidhaa au huduma inayostahili kamisheni. Kiasi cha kamisheni kinaweza kutofautiana kulingana na bidhaa au huduma husika. Points hutumika kupima shughuli na maendeleo yako kwenye mfumo, ikiwemo kushiriki kwenye Affiliate Challenges na nafasi za kupata zawadi kulingana na masharti ya challenge husika. Affiliate Wallet ndiyo sehemu ambayo unaweza kuona kamisheni na zawadi zako zilizowekwa kwenye mfumo. Unaweza kufuatilia balance yako na kufanya withdrawal moja kwa moja kwenda kwenye simu yako kulingana na taratibu zilizowekwa. Kiwango cha chini cha kutoa ni TZS 5,000, na makato ya withdrawal ni TZS 1,500 kwa muamala bila kujali kiasi unachotoa. Withdrawal zinapatikana Jumatatu hadi Ijumaa, saa 24. Kuingia kwenye Wallet, tumia email na password zilezile unazotumia kuingia kwenye Affiliate Dashboard yako. MFUMO NI RAHISI: Fanya Shughuli → Pata Mauzo → Pata Kamisheni/Points → Angalia Wallet → Withdraw Mapato Yako. KUMBUKA: Kadri unavyokuwa active katika kutangaza, kupata wateja na kufanya mauzo, ndivyo unavyoongeza nafasi yako ya kujenga kipato kupitia Kijani Asili Affiliate.

8
AFFILIATE CHALLENGE,POINTS NA ZAWADI
SOMO LA 8: AFFILIATE CHALLENGE, POINTS NA ZAWADI Kijani Asili Affiliate Challenge ni mfumo unaowapa affiliates nafasi ya kushindana, kuongeza shughuli zao na kupata zawadi mbalimbali kila wiki kulingana na performance yao. Kila wiki challenge mpya huanza, na affiliate anakusanya points kwa kutekeleza shughuli zinazotambulika kwenye challenge husika. Kadri unavyokuwa active na kukamilisha shughuli zinazohitajika, ndivyo unavyoongeza points na nafasi yako kwenye ranking ya washiriki. Mwisho wa challenge, affiliates wenye points nyingi zaidi hutambuliwa kama washindi wa wiki na kupata zawadi kulingana na nafasi zao. Zawadi za fedha huingizwa moja kwa moja kwenye Kijani Asili Affiliate Wallet na zinaweza kutolewa kwa kufuata taratibu za withdrawal. Ili kuongeza nafasi yako ya kushinda, hakikisha unaelewa sheria za challenge ya wiki, shughuli zinazotoa points, muda wa challenge na namna points zinavyohesabiwa. MFUMO NI RAHISI: Jiunge na Challenge → Tekeleza Shughuli → Kusanya Points → Panda Ranking → Shinda Zawadi → Pokea Kwenye Wallet. KUMBUKA: Challenge haijaundwa kwa ajili ya zawadi pekee — inalenga kukusaidia kuwa active, consistent na kujenga tabia ya kufanya biashara kila siku.

9
KUJENGA TEAM NA NETWORK YAKO
SOMO LA 9: KUJENGA TEAM NA NETWORK YAKO Kijani Asili Affiliate haikupi fursa ya kufanya mauzo pekee, bali pia kujenga team na mtandao wako wa biashara kwa kuwaunganisha watu wengine wenye nia ya kuwa affiliates. Anza kwa kutafuta watu wenye nia ya biashara, uwezo wa kujifunza, kufanya mauzo na kujenga mahusiano. Waelezee mfumo kwa uhalisia, waoneshe namna unavyofanya kazi na uwaongoze kufuata hatua sahihi za kujisajili. Baada ya kujiunga, kazi yako haipaswi kuishia kwenye recruitment. Wasaidie kuelewa mfumo, kutumia Dashboard, Marketing Library, link na QR Code, kutafuta leads, kufanya follow-up na kupata mauzo yao ya kwanza. Lengo ni kujenga team inayojitegemea, ambapo kila affiliate anaweza kufanya kazi, kupata wateja na kuwafundisha wengine kufanya vivyo hivyo. Kadri team yako inavyokua, zingatia mafunzo, mawasiliano, consistency, leadership na performance badala ya kuingiza watu wengi ambao hawafanyi shughuli. MFUMO WA TEAM BUILDING: Tafuta Watu → Elezea Fursa → Sajili → Fundisha → Saidia Waanze → Fuatilia Performance → Jenga Viongozi → Panua Network. KUMBUKA: Network kubwa haijengwi kwa kusajili watu pekee — inajengwa kwa kutengeneza affiliates wanaofanya kazi na viongozi wanaoweza kujenga wengine.

10
MPANGO WA KAZI NA SHERIA ZA KIJANI ASILI AFFILIATE
SOMO LA 10: MPANGO WA KAZI NA SHERIA ZA KIJANI ASILI AFFILIATE Baada ya kuelewa mfumo, hatua inayofuata ni kuufanyia kazi kwa mpango na consistency. Mafanikio yako kama affiliate yanategemea zaidi shughuli unazofanya kila siku kuliko kusubiri wateja wakufuate. Mpango wako wa kila siku uwe rahisi: tangaza content za Kijani Asili, tafuta leads wapya, jibu wanaouliza, fanya follow-up kwa leads wa zamani, tumia link au QR Code yako, fuatilia mauzo yako na endelea kujenga team yako. Jiwekee malengo ya kila siku, wiki na mwezi ya idadi ya watu unaotaka kuwafikia, leads wapya, follow-up, mauzo na affiliates wapya unaotaka kuwasaidia kuanza. SHERIA MUHIMU • Tumia taarifa sahihi kuhusu bidhaa, huduma na mfumo wa Kijani Asili. • Usitoe ahadi za uongo kuhusu afya, matokeo, kipato au kamisheni. • Usilazimishe mauzo — sikiliza mteja na mhudumie kwa heshima na weledi. • Linda taarifa za wateja na usitumie taarifa zao bila ruhusa. • Usitengeneze account feki au kufanya shughuli za udanganyifu kwa lengo la kupata points, zawadi au kamisheni. • Hakikisha account yako ime-verify na taarifa zako ni sahihi. • Fuata masharti ya challenges, commissions, Wallet na taratibu nyingine za Kijani Asili Affiliate. MFUMO WA KILA SIKU: Jifunze → Tangaza → Tafuta Leads → Zungumza → Follow-up → Funga Mauzo → Jenga Team → Rudia Kila Siku. KUMBUKA: Kijani Asili Affiliate ni biashara. Consistency, uaminifu, huduma bora na nidhamu ndiyo msingi wa kujenga network na kipato cha muda mrefu. SASA UPO TAYARI KUANZA. JENGA MTANDAO • JENGA BIASHARA • JENGA KIPATO